KIBA (Klubo internacia de Bao-amantoj)
inakualika kucheza Bao la Kiswahili katika nchi nje ya Afrika.
Anayetaka kushiriki katika mashindano haya hatakiwa kuwa
mwanachama wa chama chochote. Wachezaji watawekwa katika makundi mbalimbali
kulingana na fani zao. Ukiwa bado mwanafunzi wa mchezo huu, usikose nafasi hii
ya kukutana na wachezaji wengine na ya kujifurahisha wakati wa tamasha la GiocaRoma 2011. Tembelea tovuti ya KIBA ukitaka kucheza
kwa njia ya barua pepe na kufanya mazoezi.
Tarehe za mashindano:
Septemba 10-11, 2011.
Mahali ya mashindano:
Chama cha Michezo (Associazione Sportiva) Moon River
Via Angelo Battelli, 6
Roma
Italia
Ada:
Bado hatuna hakakia kama unatakiwa kulipa ada, lakini kama
ada ikitakuwepo haitazidi yuro 5. Mapato yatatumika kwa miradi ya
Changamano ONLUS ya kusaidia watu duni wa Tanzania.
Tarehe ya mwisho ya kujishirika:
Hamna tarehe ya mwisho ya kujishirika, lakini
tunaomba wale wanaotaka kujishirika watuandikie mapema ili tuweze kupanga
mashindano vizuri zaidi.
Muundo wa mashindano:
Muda wa kila mchezo hautaweza kuzidi dakika 90.
Zitakuwepo raundi mbalimbali kulingana na idadi ya wachezaji,
lakini hazitakuwa kuliko ya tisa.
Wachezaji watapangwa kulingana na Mfumo wa Kiswisi.
Michezo ya raundi itachezwa kwa wakati mmoja.
Kalenda ya raundi itakuwa kama inavyofuata:
Jumamosi, Septemba 10:
04:00 - 05:30 : raundi ya 1
05:30 - 07:00 : raundi ya 2
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 3
09:30 - 11:00 : raundi ya 4
11:00 - 12:30 : raundi ya 5
Jumapili, Septemba 11:
04:00 - 05:30 : raundi ya 6
05:30 - 07:00 : raundi ya 7
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 8
09:30 - 11:00 : raundi ya 9
12:00 : Utoaj rasmi wa matuzo
Matuzo:
Tuzo la 1 halijachaguliwa
Tuzo la 2 hati
Tuzo la 3 hati
Maelezo zaidi:
Ili kupata maelezo mengine na kujiandikisha tafadhali andika kwa
info@tavolando.net
au info@kibao.org
au info@changamano.org.