Wakati wa Gioca Torino 2009

Novemba 21-22, 2009

 KIBA

Klubo Internacia de Bao Amantoj

inaandaa Mashindano ya Kimataifa la Mchezo wa Bao

 Bao

Wanaruhuswa kushiriki wachezaji wa Italia na wa nchi nyingine.


LaKIBA (Klubo internacia de Bao-amantoj) inakualika kucheza Bao la Kiswahili katika nchi nje ya Afrika.

Anayetaka kushiriki katika mashindano haya hatakiwa kuwa mwanachama wa chama chochote. Wachezaji watawekwa katika makundi mbalimbali kulingana na fani zao. Ukiwa bado mwanafunzi wa mchezo huu, usikose nafasi hii ya kukutana na wachezaji wengine na ya kujifurahisha wakati wa tamasha la Gioca Torino 2009. Tembelea tovuti ya KIBA ukitaka kucheza kwa njia ya barua pepe na kufanya mazoezi.

Tarehe za mashindano:

Novemba 21-22, 2009.

Mahali ya mashindano:

Kituo cha Maduka (Centro commerciale) [8]Gallery Lingotto
via Nizza 230
Torino
Italia

Ada:

Ada ni yuro 5. Mapato yatatumika kwa miradi ya Changamano ONLUS ya kusaidia watu duni wa Tanzania.

Tarehe ya mwisho ya kujishirika:

Hamna tarehe ya mwisho ya kujishirika, lakini tunaomba wale wanaotaka kujishirika watuandikie mapema ili tuweze kupanga mashindano vizuri zaidi.

Muundo wa mashindano:

Muda wa kila mchezo hautaweza kuzidi dakika 90.

Zitakuwepo raundi mbalimbali kulingana na idadi ya wachezaji, lakini hazitakuwa kuliko ya tisa.

Wachezaji watapangwa kulingana na Mfumo wa Kiswsi.

Michezo ya raundi itachezwa kwa wakati mmoja.

Kalenda ya raundi itakuwa kama inavyofuata:

Jumamosi, Novemba 21:
04:00 - 05:30 : raundi ya 1
05:30 - 07:00 : raundi ya 2
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 3
09:30 - 11:00 : raundi ya 4
11:00 - 12:30 : raundi ya 5

Jumapili, Novemba 22:
04:00 - 05:30 : raundi ya 6
05:30 - 07:00 : raundi ya 7
Chakula cha mchana 07:00-07:30
08:00 - 09:30 : raundi ya 8
09:30 - 11:00 : raundi ya 9
12:00 : Utoaj rasmi wa matuzo

Matuzo:

Tuzo la 1 Mchezo mmoja wa Bao kutoka Tanzania
Tuzo la 2 (halijachaguliwa)
Tuzo la 3 (halijachaguliwa)

Maelezo zaidi:

Ili kupata maelezo mengine na kujiandikisha tafadhali andika kwa   info@tavolando.net au info@kibao.org au info@changamano.org.

Wanaotaka kufanya mazoezi ya mchezo wa Bao wanaweza kwenda kwa

www.kibao.org/




Bonyeza hapa ukitaka kurudi kwa Tavolando.net